Home Makala Ahou Apindua Meza

Ahou Apindua Meza

by Sports Leo
0 comments

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba Sc Jean Charles Ahoua amepindua meza na sasa anaongoza safu ya ufungaji bora ya ligi kuu ya soka ya Nbc nchini.

Ahoua sasa anashikilia usukani akiwa na mabao 15 na assisti saba baada ya jana kufunga mabao matatu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Klabu ya Pamba Jiji Fc uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Kwa muda mrefu safu hiyo ya ufungaji bora walikua wakipishana mastaa wa Yanga Sc Prince Mpumelelo Dube na Clement Mzize ambao sasa wamesimama wakiwa na mabao 13 kwa Mzize huku Dube akiwa na mabao 12.

banner

Lakini baada ya Simba Sc kuanza kucheza michezo yake ya viporo ambapo Ahoua mara nyingi amekua akianzia benchi au kutocheza kabisa mpaka hapo jana alipopewa nafasi ya kuanza na kufunga mabao hayo matatu.

Kwa mujibu wa takwimu mpaka sasa Ahoua ana nafadi kubwa ya kuibuka mfungaji bora kutokana na idadi kubwa ya mabao pamoja na kusaliwa na michezp minne kwa klabu yake ya Simba sc.

Huku pia kuna nafasi kubwa msimu huu kwa staa atakayepata tuzo hiyo pia kupata tuzo ya mchezaji bora wa msimu huu wa ligi kuu ya Nbc nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited