Home Makala Amunike Amvaa Fei Toto

Amunike Amvaa Fei Toto

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania(Taifa stars) Emmanuel Amunike amemvaa kiungo wa Yanga Feisal Salum “Fei toto” juu ya kadi za njano anazopata mara kwa mara.

Kocha huyo mnigeria ameamua kufunguka kukerwa kwake na idadi ya kadi wanazopata viungo wake hasa Feisal kuwa kadi hizo hazina afya kwa timu na amepanga kulifanyia kazi suala hilo kwa timu nzima na si kwa mchezaji mmoja.

Amunike amesisitiza kulifanyia kazi suala hilo kwa Feisal kwa kuwa ni tatizo la muda mrefu na limeanzia klabuni kwake Yanga sc na amepanga kukutana na mchezaji huyo ili kumpa ushauri.

banner

Amunike mchezaji wa zamani wa Barcelona ya Hispania aliongoza stars katika mechi ya kwanza ya Afcon dhidi ya senegali ambapo stars ilizidiwa idara ya kiungo na kuwafanya viungo wake wakiongozwa na Feisal kuishia kucheza faulo na kupata kadi za njano.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited