Mabosi wa klabu ya Azam Fc wamefikia makubaliano ya kutemana na kocha wao Rashid Taoussi pamoja na benchi lake la ufundi baada ya kuona kocha huyo hajafikia malengo ya klabu.
Taarifa za uhakika ni kuwa Azam tayari wamepata kocha mpya kuelekea msimu ujao, ila makubaliano ya Azam na kocha Taoussi ni kumaliza huu msimu huu huku tayari akiwa amelipwa stahiki zake zote.
Azam Fc inaona kama kocha huyo hana tena maajabu baada ya kukaa msimu mmoja klabuni hapo na sasa inasubiri mkataba wake uishe ili waachane salama salmini.
Kuelekea msimu ujao pamoja na kuwa tayari imempata kocha mpya na tayari imeanza usajili ya mastaa wapya klabuni hapo ambapo tayari imemsajili kipa Aishi Manula ambaye anakuja kuchukua nafasi ya Mohamed Mustapha ambaye ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.