Klabu ya Azam Fc imeachana na kiungo wake Franklin Navaro kwa makubaliano ya pande mbili baada ya kocha Rachid Taoussi kutoridhishwa na uwezo wa staa huyo mazoezini.
Navaro aliingia na bahati mbaya kikosini ambapo aliumia dakika chache katika mchezo wake wa kwanza wa klabu hiyo katika michuano ya kombe la Mapinduzi Visiwani Zanzibar.
Baada ya kuumia staa huyo alipelekwa nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya matibabu na tangu hapo aliondolewa katiks usajili wa wachezaji wa kigeni klabuni hapo baada ya kugundulika kuwa matibabu yake yatachukua muda mrefu zaidi.
Sasa staa huyo mwenye miaka 25 amerejea mazoezini ambapo baada ya kumfanyia tathmini kocha Rachid Taoussi amewataka mabosi wa klabu hiyo kuachana na staa huyo kwa sababu za kiufundi huku akiwataka kusajili mastaa wa maana zaidi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mbali na Navaro pia mabosi wa klabu hiyo wanaangalia uwezekano wa kuachana pia na mshambuliaji Jhonier Blanco kutokana na kocha kutoridhishwa na uwezo wake ambapo kwa sasa anamtegemea Nassoro Saiduni pekee.
Tayari mabosi wa Azam Fc wameanza kusajili baadhi ya mastaa kuboresha kikosi hicho wakimsajili Zidane Seleli na Landry Zouzoua.