Home Makala Azam Fc Yashusha Straika Mashine

Azam Fc Yashusha Straika Mashine

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam Fc imemsajili mshambuliaji Jhonier Blanco kutoka klabu ya Fortaleza CEIF inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Colombia kwa mkataba wa miaka minne akichukua nafasi ya Prince Dube ambaye ameonyesha nia ya kuvunja mkataba na klabu hiyo.

Mshambuliaji huyo amewahi kuwa mshambuliaji bora katika ligi hiyo ya daraja la kwanza nchini Colombia maarufu kama “Categoría Primera B” ambapo alifanikiwa kufunga jumla ya mabao akifunga mabao 13, msimu uliopita 2022/23 na alifanikiwa kuisaidia Fortaleza kupanda daraja na kuchukua ubingwa, huku akihitimisha msimu huo kwa rekodi nzuri baada ya kufunga jumla ya mabao 18 kwenye mechi 26 za mashindano yote.

Azam Fc msimu ujao itashiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika ambapo itakutana na timu nyingi bora zenye vikosi ghali na wachezaji wazoefu hivyo inahitaji kuwa na kikosi kipana na kinachokidhi mahitaji ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya vilabu Afrika.

banner

Mpaka sasa Azam Fc imeshakamilisha usajili wa mchezaji mwingine kutoka America ambaye ni Ever William Meza na usajili huu unakua wa pili wa kimataifa ambapo pia ina mpango wa kuachana na mastaa kadhaa wa kimataifa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited