Home Makala Azam Fc Yatinga Nusu Fainali Shirikisho

Azam Fc Yatinga Nusu Fainali Shirikisho

by Sports Leo
0 comments

Baada ya kufanikiwa kuifunga 2-0 timu ya Mtibwa Sugar sasa klabu ya Azam Fc imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho nchini ambalo linaendelea kwa michezo mingine ya nusu fainali wikiendi hii.

Azam Fc ikicheza katika uwanja wake wa nyumbani wa Chamazi Complex ilifanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya 28 likifunga na Kipre Jr akimalizia mpira ambao mabeki wa Mtibwa Sugar walizembea kuokoa na kumkuta mfungaji akiwa katika nafasi nzuri bila bughudha.

Timu hizo ziliingia kipindi cha pili zikiwa na matokeo ya 1-0 lakini dakika ya 74 Abdul Sopu alifanikiwa kuwatuliza Mtibwa Sugar akiwafunga bao la pili lililowamaliza nguvu na kuufanya mchezp huo kumalizika kwa mabao hayo kwa Azam Fc.

banner

Sasa Azam Fc inasubiri mshindi kati ya Simba sc dhidi ya Ihefu ili kufahamu nani itacheza nae hatua ya nusu fainali ambapo klabu hizo zitamenyani ijumaa katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited