Azam Fc imezidi kujiwekea rekodi nzuri ndani ya msimu huu mpya wa ligi kuu bara 2020/2021 baada kufika raundi ya sita pasipo kufungwa wala kutoa sare ya kufungana.
Kikosi hicho kinachoongozwa chini ya kocha mkuu, Arstica Ciaoba kimefikisha jumla ya pointi 18 baada ya kunyakua pointi 3 hapo jana Octoba 15, kwa kuwatungua Mwadui Fc 3-0 uwanja wa Azam Complex.
Mabao mawili ya Azam Fc yalipachikwa na Obrey Chirwa dakika ya 28 na 63 huku yule kinara wao wa mabao Prince dube alitupia bao dakika ya 61.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Azam Fc kwa sasa inashika usukani ikiwaacha mabingwa watetezi wa ligi kuu bara,Simba Sc nafasi ya pili wakiwa na pointi 13 kibindoni katika michezo mitano waliocheza nakufunga mabao 14 pekee kupitia safu yao ya ushambuliaji.