Wakati Yanga Sc ipo kwenye anga ya kufanya maboresho ya kikosi chake ili kuwa na ushindani kwenye namba zote kuanzia kipa mpaka wachezaji wa ndani, vita yao sasa inaongezewa makali na Azam Fc ambao wameshapaki basi lao ndani ya Kagera Sugar wakianza na Awesu Awesu ambaye ni kiungo aliyekuwa pia kwenye rada za Yanga.
Mabosi wa Yanga wapo kwenye jitihada za kumvutia kasi kipa namba moja wa Kagera Sugar, Benedickt Tinoco ili aongeze nguvu katika kikosi chao msimu ujao kwani hawakuwa na msimu mzuri ndani ya 2019/20.
Antonio Nugaz ambaye ni ofisa uhamasishaji wa Yanga amesema kuwa Tinoco wa Kagera Sugar ni kipa mwenye uwezo mkubwa na anakubalika hivyo anaweza kuibukia Yanga siku ya Mwanachi akaendeleze kutoa changamoto kwa Metacha Mnata, Faroukh Shikhalo na Ramadhan Kabwili.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.