Aliyekuwa beki wa Simba Sc Zana Coulibaly ambaye pia ni raia wa Ivory Coast amesema kuwa yupo tayari kurejea Bongo kukipiga ndani ya Yanga auAzam iwapo watahitaji huduma yake.
Beki huyo alidumu Simba kwa miezi tisa kabla ya kuondoka na kujiunga na AS Vita ya DR Congo kwa mkataba wa miaka miwili katika michuano ya kimataifa amefanikiwa kucheza mechi tatu pekee msimu huu.
Coulibaly amesema kuwa moja kati ya sehemu ambazo hawezi kuzisahau kirahisi ni Tanzania na yupo tayari kurejea kwa kujiunga na timu yoyote zikiwemo Azam na Yanga kutokana na ukarimu wa watu wake.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
“Natamani kuona narudi tena huko kucheza haijalishi ni timu gani iwe kama Azam au hata Yanga wakinihitaji nitakuwa tayari kurejea,” amesema Coulibaly.