Home Makala “Bado Tunachunguza”TPLB

“Bado Tunachunguza”TPLB

by Sports Leo
0 comments

Bodi ya ligi kuu nchini (Tplb) imesema kuwa bado inafanya uchunguzi juu ya vitendo vya rushwa na ukosefu wa  usalama vilivyopelekea kuahirishwa kwa mchezo baina ya Yanga sc dhidi ya Simba Sc Machi 8 2025.

Mchezo huo uliahirishwa na bodi hiyo baada ya kutokea sintofahamu ambapo klabu ya Simba Sc iligomea mchezo huo baada ya kuzuiwa kufanya mazoezi siku moja kabla ya mchezo.

banner

Akizungumza mapema hii leo mtendaji mkuu wa bodi hiyo Almas Kasongo alisema kuwa mpaka sasa bado uchunguzi haujakamilika ndio maana hawajatoa mrejesho.

“ Neno uchunguzi ni neno pana na inawezekana katika taarifa yetu hatukueleza wazi ni uchunguzi wa aina gani unafanywa na unakusudiwa na hata watu kutaka kufahamu wanastahili pia ni haki yao”.

“Cha kwanza kwa maana ya uchunguzi lile tukio tukalipeka kwa kamati na kamati ikafanya maamuzi na baada ya hapo tuliitwa na vyombo vyenye dhamana ya kufanya hayo mambo na walituuliza mambo mengi na jambo letu tunaimani limepokelewa hilo jambo na sisi tulizungumza yale yote yaliyotokea siku ya tukio na wakaridhika na sasa bado wanaendelea nalo”,Alisema Kasongo.

“Na naamini pale watakapo kuwa tayari watakuja na majibu na ukirudi kwetu sasa wahusika wote kwanzia wasimamizi wa kanuni za ligi kwa ujumla unaweza kuona kwa namna moja ama nyengine kama tutajiridhisha basi kanuni za ndani zitafanyika ya kazi”Alisema huku akiendelea kuwa.

“Sisi kama bodi tumemaliza uchunguzi wetu maana tulipokea taarifa zote rasmi zinazohitajika itoshe kusema taarifa zote tunazo na hilo shauri tayari lipo kwenye kamati na kikao kijacho kamati itatoa majibu kwa wahusika na kamati ikijiridhisha na taarifa tulizozikusanya na mazingira ya video kamati itajadili na itafanya maamuzi”.Alimalizia kusema Kasongo

Mchezo huo umeleta mijadala katika mitandao ya kijamii baada ya wadau wa michezo kuhoji kitendo cha bodi hiyo kuupangia tarehe 15 juni 2025 kuwa siku ya kuchezwa ikiwa mpaka sasa suluhu haijapatikana.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited