Kiungo wa Yanga Mapinduzi Balama ameibuka mchezaji bora wa mechi ya watani wa jadi Simba sc na Yanga baada ya kuonyesha kiwango bora na kupelekea kupewa tuzo ya mchezaji bora kwa upande wa klabu yake.
Balama aliyefunga bao la kwanza lililoirudisha Yanga mchezoni mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya kuwa imetanguliwa kufungwa mabao 2.
Licha ya kufunga pia mchezaji huyo alionyesha uwezo mkubwa katika kiungo cha timu hiyo na hivyo kupewa zawadi ya godoro kutoka kwa wadhamini wa klabu hiyo kampuni ya Gsm kupitia magodoro ya Gsm Foam.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.