Namungo Fc imekamilisha usajili wa aliyekuwa beki wa Yanga Sc, Jaffar Mohammed kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Usajili wa beki huyo unaenda kuongeza nguvu eneo la ulinzi kwa lengo la kuhakikisha wanakuwa imara kuelekea mashindano ambayo Namungo Fc itashiriki kuiwakilisha Afrika kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Namungo Fc ilipata fursa hiyo baada ya kushika nafasi ya pili kwenye fainali za kombe la shirikisho la Azam (ASFC) ambapo ubingwa ulichukuliwa na Simba Sc.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.