Home Makala Beki Yanga sc Akutwa na Mazito

Beki Yanga sc Akutwa na Mazito

by Dennis Msotwa
0 comments

Beki mpya wa klabu ya Yanga sc Gift Fred ameondolewa kwemye kikiosi cha timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) baada ya kubainika kuwa  majeraha muda mchache kabla ya kikosi cha timu hiyo kutangazwa hadharani.

Iko hivi beki huyo mwenye mwili wa miraba minne tayari alikua ameshatumiwa barua ya kuitwa kikosini huku klabu yake ikiwa tayari imetoa taarifa rasmi kuwa ni miongoni mwa mastaa walioitwa kujiunga na timu zao za taifa lakini baada ya jopo la matabibu wa timu ya taifa kukaa na kufanya tathmini waligundua kuwa beki huyo ana majeraha na hivyo kuamua kumpa muda wa kujitibu.

Kocha Micho baada ya kupata taarifa hiyo alitangaza kikosi hicho kwa waandishi wa habari pasi kulijumlisha jina la beki huyo hivyo kuzua sintofahamu.

banner

“Gift Fred ni miongoni mwa wachezaji wetu (12) walioitwa kwenye timu mbalimbali za taifa .. Fred akiwa kwenye mazoezi na timu yake ya taifa ya Uganda alipata minor injury (Injury ndogo) ambayo ingemuweka nje kwa siku 3 hadi 4”.Alisema mkuu wa Idara ya habari ya klabu ya Yanga sc Ally Kamwe.

“Madaktari wa timu ya taifa ya Uganda wametutaarifu kuwa wamemruhusu Gift Fred kurejea Tanzania na kocha ameshaita mbadala wake kuelekea mechi yao ya kufuzu Afcon dhidi ya Niger”.Aliendelea kusema.

“Kikosi kimetoka jana public tayari Fred alikuwa ameshaondolewa kwenye squad baada ya kupata injury”

Pia alibainisha kuwa beki huyo atarudi nchini kesho kwa ajili ya kuendelea na program za kujiweka fiti huku akikanusha kabisa kuwa taarifa za kwamba hakuitwa sio sahihi “Taarifa kwamba hakuitwa ni uongo kwani call-ups zote za wachezaji kwenye timu zao za taifa hupitia (TFF)”.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited