Kamati maalumu ya usimamizi wa ligi kuu chini ya bodi ya ligi kuu nchini imempiga faini ya shilingi milioni mbili aliyekua kocha wa klabu ya Yanga sc Miguel Gamondi kwa kosa la kumsukuma kocha msaidizi wa klabu ya Singida Black Stars Sliman Marloen katika mchezo wa ligi kuu namba 32 uliofanyika katika uwanja wa New Amaan complex Visiwani Zanzibar.
Katika mchezo uliokua na presha kwa pande zote ambapo Yanga sc ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 lililofungwa na Pacome Zouzoua ambapo kulikua na kurushiana maneno baina ya mabenchi ya ufundi wa timu hizo na ndipo Gamondi alipofanya kosa hilo.
Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 45:2(2:1) ya ligi kuu nchini ambapo sambamba na kupigwa faini hiyo pia ataikosa michezo mitatu ya ligi kuu nchini ama michuano ya kombe la Shirikisho la Crdb.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Hata hivyo Gamondi tayari ameshatimuliwa klabuni hapo hivyo kuna adhabu atazikwepa kwa sasa.