Rasmi klabu ya Yanga sc imetangaza kuachana na Mkuu wa Idara ya Habari ya klabu hiyo Hassan Bumbuli baada ya mkataba wake kumalizika na klabu kuamua kutoendelea nae.
Yanga sc imetangaza kumtakia kila la kheri Bumbuli katika majukumu yake mapya mahala pengine huku pia ikisemekana kuwa nafasi hiyo itatangazwa kupitia vyombo vya habari ili watu watume maombi ya kuziba nafasi hiyo.
Bumbuli amefanya kazi klabuni hapo kwa muda wa miaka mitatu huku akifanikiwa kumudu hali ngumu ya uchumi wa klabu hiyo kabla ya kuingia kwa Gsm ambaye ameleta neema ya fedha klabuni hapo na kurejesha furaha kwa mashabiki wa klabu hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Tangu aingie Rais mpya wa klabu hiyo Eng.Hersi Said amekua akifanya mabadiliko klabuni hapo akiwatoa baadhi ya maafisa klabuni hapo ambapo alianza na Mkurugenzi wa Mashindani Thabit Kandoro ambaye nafasi yake imechukuliwa na Saad Kawemba huku Walter Harrison akichukua nafasi ya Meneji Hafidh Salehe ambaye amehamishwa kuwa mratibu wa timu.