Home Makala Casemiro Aikoa United

Casemiro Aikoa United

by Dennis Msotwa
0 comments

Jahazi lilikua limeshazama kwa Manchester United ambao walilazimika kusawazisha dakika za mwishoni za mchezo wa ligi kuu dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge ambapo makosa ya kiungo Scott Mctominay yaliwapa Chelsea bao la penati dakika ya 87 likifungwa na Jorginho.

ikianza na kiungo Casemiro na Fred huku Anthony,Sancho na Rashford wakianza eneo la mbele dhidi ya Thiago Silva,Challobah na Cucurella huku eneo la ushambuliaji likiwa na Aubemayang,Sterling na Mason Mount.

Man United ilitawala kipindi cha kwanza huku kuingia kwa Matteo Kovacic kuliibadili Chelsea na kufanya mashambulizi makali kwa United baada ya kupata balansi katika eneo la kiungo.

banner

Jorginho alifunga kwa penati hiyo baada ya Mc Tominay kumkumbatia wakati akipambana kufunga kwa kona ambapo bao hilo lilisawazishwa na Casemiro kwa kichwa akiunganisha krosi kutoka upande wa kulia mwa uwanja dakika ya 90+4 na kufanya mechi kumalizika kwa sare ambapo sasa Chelsea imefikisha alama 21 katika michezo 11 na Man utd imefikisha alama 20 katika michezo 11 ya ligi kuu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited