Home Makala Chama Atwaa Tuzo Simba sc

Chama Atwaa Tuzo Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba sc Cletous Chama ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi August wa klabu hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Emirates Alluminium akiwashinda mastaa wawili Pape Osmane Sakho na Sadio Kanoute.

“Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Simba Profile Fans Player of the Month) kwa mwezi Agosti, 2022 inakwenda kwa Clatous Chama,”Ilisomeka taarifa kutoka klabuni hapo ikieleza juu ya ushindi huo.

Katika mwezi uliopita Chama alikua na mchango mkubwa katika kikosi hiko akifanikiwa kufunga bao moja kutoa pasi moja ya bao na kasababisha faulo moja iliyoleta bao ilikuwa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Geita Gold, Simba iliposhinda mabao 3-0.

banner

Chama msimu huu ameonekana kurejesha kiwango chake baada ya kutokua na msimu mzuri uliopita ambapo alijiunga na Simba sc akitokea Rs Berkane ambapo alishindwa kupata namba na kusababisha klabu hiyo kumuuza kuja Simba sc.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited