Timo Werner anayetupia ndani ya klabu ya RB Leipzig yupo kwenye hesabu za Chelsea pamoja na Liverpool ambao wanapambana kuipata saini ya nyota huyo ili kuimarisha vikosi vyao msimu ujao.
Liverpool iliyo chini ya Jurgen Klopp inahaha kutafuta mbadala wa Sadio Mane ambaye inaelezwa kuwa Real Madrid inamuhitaji huku Chelsea iliyi chini ya Frank Lampard pia ikisaka mtupiaji.
Werner amekuwa kwenye ubora wake ndani ya Rb Leipzig akiwa ana mabao 27 katika mechi 37 alizocheza.