Home Makala Chico Arejea Yanga sc

Chico Arejea Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Winga raia wa Congo Chico Ushindi amerejea kutoka majeruhi klabuni Yanga sc baada ya kuumia misuli katika mchezo dhidi ya Kmc ambao klabu yake iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 uliofanyika katika uwanja wa Taifa.

Mchezo huo ulikua ni wa kwanza kwa winga huyo kuanza katika kikosi cha kwanza tangu asajiliwe akitokea Tp Mazembe ya mjini Lubumbashi nchini Congo ambapo alisaidia kupatikana kwa bao la pili baada ya kupiga kona iliyomkuta Djuma Shabani ambaye alifunga kwa kichwa na kuiandikia Yanga sc bao la pili.

Chico tangu asajili amekua akisumbuliwa na majeraha ya misuli ambayo inaashiria hakua na utimamu wa mwili wa kutosha wakati anajiunga na klabu hiyo yenye makombe mengi ya ligi kuu nchini kuzidi klabu yeyote.

banner

Daktari maarufu wa viungo wa Yanga sc ameonekana katika viwanja vya mazoezi ya timu hiyo vilivyoko Avic Town Kigamboni ambapo Chico alikua akifanya mazoezi ya kujenga utimamu huo kwa kuruka koni na kukimbia mbio fupi fupi japo inaonekana hataweza kuikabili Namungo siku ya tarehe 23 lakini anaweza kuwepo katika mchezo dhidi ya Simba sc April 30.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited