Home Makala Chico,Yacouba kuwakosa Simba sc

Chico,Yacouba kuwakosa Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga sc Cedrick Kaze amesema kuwa wachezaji Chico Ushindi na Yacouba Songne wataukosa mchezo wa kesho wa ligi kuu nchini dhidi ya Simba sc utakaofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa saa 11 jioni.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaze alisema kuwa Chico na Yacouba wataukosa mchezo huo kutokana na kukosa utimamu wa mechi baada ya kuwa na majeraha ya muda mrefu hivyo kuhitaji muda kukaa sawa japo walishapona majeraha.

kesho dhidi ya Simba sc tutakuwa na kikosi kamili baada ya wachezaji wetu Saido Ntibanzokiza na Djuma Shabani ambao walikuwa majeruhi wamepona na wapo tayari kwa mchezo huku wachezaji pekee ambao tutawakosa ni Yacouba Sogne na Chiko Ushindi”.

banner

Yanga sc itaingia katika mchezo huo ikiwa na matumaini ya kuendeleza gepu la alama 13 katika yake na Simba sc ili kutengeneza mazingira ya kutwa taji la ligi kuu mapema ikiwa imelikosa taji hilo kwa miaka minne mfululizo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited