Benchi la ufundi la Juventus limethibitisha kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ambaye ni mchezaji pia wa mabingwa hao wa ulaya amekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona.
Ronaldo kwa sasa yupo chini ya uangalizi maalum wa madaktari kwaajili ya kurudisha afya yake ya awali kwa kuwa ni mchezaji pekee aliyeambukizwa virusi hivyo japo hakuonyesha dalili zozote za Covid 19.
Staa huyo ataukosa mchezo muhimu wa kundi C leo Octoba 14, kati ya Ureno dhidi ya Sweden utakaochezwa katika uwanja wa Avalade, katika mbio za kuwania kufuzu mashindano ya Uefa Nation League.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.