Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Stephane Aziz Ki amechelewa mchezo dhidi ya Ruvu Shooting baada ya kugundulika kuwa ana maambukizi ya virusi vya Covid 19 katika nchi ya Morroco aliposhikiliwa na kumfanya akose mchezo wa ligi kuu nchini dhidi ya Ruvu Shooting uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Aziz Ki kiungo kipenzi cha mashabiki wa klabu ya Yanga sc alishikiliwa nchini Morocco kutokana na kukutwa na maambukizi ya virusi vya Covid 19 ambapo alipaswa kupewa matibabu kwa siku kadhaa na baadae alibainika kuwa amepona na ndipo aliporuhusiwa kujiunga na kambi ya Yanga sc iliyoanza jana baada ya kutua nchini ambapo kuna asilimia kubwa kuwa atashiriki katika mchezo dhidi ya Al Hilal ya Sudan siku ya Jumamosi.
Kiungo raia wa Bukina Faso alikuwa alisafiri kwenda nchini alipokwenda kuitumikia timu yake ya Taifa katika michezo miwili ya kirafiki iliyokuwa kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) ambapo baada ya vipimo na kugundulika kuwa na maambukizi ilimlazimu kusubiri kwa siku kadhaa baada ya matibabu ili kuhakikisha anapona kabisa na kuruhusiwa kuendelea safari na ndipo aliporuhusiwa na kufanikiwa kutua nchini.
Kuwasili kwa mchezaji kunampa unafuu mkubwa bosi wa ufundi wa klabu hiyo Nasreddine Nabi kuwa na machaguo ya kutosha katika eneo la kiungo anapoelekea katika mcheo huo mgumu kabisa wa ligi ya mabingwa barani Afrika siku ya Jumamosi October 8.
Â