Patrick Gakumba ambaye ni wakala wa nyota wa Simba Sc, Meddie Kagrer amefunguka kwamba dili la mchezaji wake kutakiwa na klabu ya Hispania limekuwepo na kitu pekee ambacho kinakwamisha suala hilo ni mabosi wa Simba.
Wakala huyo alipata dili hilo baada ya kuzungumza na rafiki yake ambaye anaishi Hispania ambapo alikuwa anataka ampeleke straika huyo kwa ajili ya mkopo ambao angeweza kununuliwa moja kwa moja.
Licha ya jina la klabu hiyo kufichwa, inaelezwa kuwa ni Levante ndiyo inayomhitaji straika huyo na endapo dili hilo litashindikana litafanya kagere kukosa fedha nyingi.