34
Mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube, anatarajiwa kuwa nje ya dimba kwa muda wa wiki mbili zijazo baada ya kupata majeraha ya misuli ya nyama za paja za mguu wake wa kushoto.
Dube aliumia dakika ya 25 kwenye mchezo wa VPL dhidi ya Mwadui uliopigwa dimbani Mwadui Complex, Jumamosi Machi 6.
Kwa mujibu wa taarifa za klabu hiyo mshambuliaji huyo raia wa Zimbabwe atapumzika kabisa kwenye wiki yake ya kwanza ya matibabu kabla ya kuanza mazoezi mepesi katika wiki ya pili ya mwisho ya kutibu majeraha hayo.