Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) imemfungia miaka miwili aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga Sc , Luc Eymael kujihusiana na masuala ya soka Tanzania pia kutozwa faini ya Shilingi milioni 8.
Eymael amekutana na pigo hili kutokana na makosa ya ubaguzi pamoja na uchochezi ambao aliufanya baada ya mchezo wa mwisho wa ligi kuu bara dhidi ya Lipuli uliochezwa Julai 26 Uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Kosa hilo lilimpelekea kocha huyo Mbelgiji kufufutwa rasmi kazi na Yanga, Julai 27 na kwa sasa yupo zake Ubelgiji.