Mastaa wawili wa klabu ya Yanga sc Farid Mussa na Yao Kouasi Attouhoula wanatarajiwa kuukosa mchezo wa Ufunguzi wa ligi kuu kwa klabu yao dhidi ya Kagera Sugar Fc utakaofanyika August 29 katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.
Kikosi cha Yanga sc tayari kimewasili mkoani humo huku mastaa hao wakiachwa jijini Dar es Salaam kutokana na kusumbuliwa na majeraha ambapo Yao mpaka sasa anaendelea vizuri na yupo karibuni kurejea kikosini.
Kwa upande wa Farid Mussa yeye anatarajiwa kufanyiwa upasuaji ili kupona jeraha lake ambapo anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kikosi cha Yanga sc baada ya kumaliza michuano ya kimataifa ya klabu bingwa barani Afrika hatua ya awali sasa kimerejea kwa ajili ya ligi kuu nchini na kitavaana na Kagera Sugar katika mchezo huo wa kwanza wa ligi msimu huu.