Home Makala Fei Toto Arejea TFF

Fei Toto Arejea TFF

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa klabu ya Yanga sc Feisal Salum amerejea katika makao makuu ya shirikisho la soka nchini yaliyoko Karume jijini Dar es salaam akiomba kuvunjwa kwa mkataba wake na klabu ya Yanga sc ambao mpaka sasa umebakiza takribani mwaka mmoja na nusu.

Kiungo huyo aliwasili akiwa na mwanasheria wa kimataifa wa kesi za wachezaji aitwae Jasmine ambaye alisema kuwa wamekuja kuwasilisha ombi la kuvunja mkataba na klabu ya Yanga sc kwani mchezaji huyo hana nia ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Feisal hapo awali alivunja mkataba wake na klabu hiyo bila kufuata utaratibu sahihi hivyo kuilazima kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kumuamuru arejee katika klabu yake ya Yanga sc ambapo mchezaji huyo hakurejea bali aliomba barua ya marejeo ya kesi husika ambapo pia marejeo hayo hayakubadilisha hukumu hiyo ya awali ya kumtaka arejee klabuni kwake.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited