Home Soka Feisal Ageuka Lulu Afrika Kusini

Feisal Ageuka Lulu Afrika Kusini

by Sports Leo
0 comments

Ripoti kutoka Afrika Kusini zinaeleza kuwa kiungo wa Azam FC,Feisal Salum yupo katika rada za klabu ya Kaizer Chiefs ambayo inanolewa na Nassredine nabi ambaye aliwahi kufanya nae kazi wakati huo wakiwa Young Africans pamoja na Cedric Kaze ambaye kwa sasa ni msaidizi wa Nabi.

Inaelezwa kuwa Nabi anahitaji kuongeza nguvu katika kikosi hicho na eneo ambalo anahitaji kuliongezea nguvu ni eneo la kiungo na kwa kushirikiana na Msaidizi wake Kaze wameona Feisal atakuwa tiba eneo hilo.

Wanautambua uwezo wa Feisal tangu akiwa Young Africans na sasa Azam na wamefanya kazi pamoja kwa muda kiasi.

banner

Mbali na Kaizer Chief,Pia miamba mingine kutoka Afrika kusini Mamelodi Sundowns wanamnyatia kiùngo huyo fundi kutoka Tanzania na klabu ya Azam.

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka Afrika kusini,Gharama ya kumnasa Feisal huenda ikawa kikwazo kwa miamba hiyo,Bado Ofa rasmi haijatumwa kwa uongozi wa Azam juu ya uhitaji wa huduma ya Feisal salum.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited