Home Makala Halaand Kutua Man City

Halaand Kutua Man City

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Manchester City imezishinda klabu ya Barcelona na Real Madrid kuwania saini ya mshambuliaji wa klabu ya Borrusia Dortmund Erlin Halaand baada ya kukubaliana na klabu ya Borrusia Dortmund kumsaini staa huyo kwa dau linalokadiriwa kufikia kiasi cha  paundi milioni 50.

Awali klabu ya Real Madrid ilikua mstari wa mbele kukamilisha dili hilo lakini Man city wamewapiga bao na kutangaza usajili huo wa Halaand ambaye atakwenda kulipwa dola 375,000 kwa wiki huku akiingia katika orodha ya mastaa wanaolipwa zaidi klabuni hapo sambamba na Kelvin De Bryne.

Tayari Man city imetangaza kukamilika kwa dili hilo huku staa huyo akitarajiwa kujiunga na timu hiyo mwezi julai mwaka huu katika kipindi cha majira ya joto huku kocha Pep Guardiola akipata nafuu baada ya mabosi wa klabu hiyo kushindwa kukamilisha dili la mshambuliaji wa Tottenhan Hotspurs Harry Kane msimu uliopita.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited