Aliyekua kocha wa klabu ya Yanga sc Miloud Hamdi Aibuka Kocha Bora Juni 2025 akiwashinda makocha Rachid Taoussi wa Azam Fc na Fred Felix Minziro wa Pamba Jiji Fc ambao aliingia nao fainali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya ligi kuu nchini kocha huyo ametwaa tuzo hiyo baada ya kuiongoza Yanga sc kushinda michezo mitatu ya ligi kuu ya Nbc nchini na kuisaidia kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Nbc.
Tuzo hiyo hutolewa kila mwezi ambapo kamati maalumu iliyoundwa kusimamia tuzo hizo hukutana na kufanya tathmini ya kina na kupitia takwimu ili kupata mshindi.
Miloud tayari ameachana na klabu ya Yanga sc na amejiunga na klabu ya Ismailia ya nchini Misri baada ya mkataba wake kutamatika akiingoza Yanga sc kutwaa mataji matatu ya ndani msimu huu.
Â