Home Makala Hatarii-Simba Yazidi Kuweka Alama Kimataifa

Hatarii-Simba Yazidi Kuweka Alama Kimataifa

by Sports Leo
0 comments

Simba Sc imezidi kuweka alama kimataifa baada ya mtendaji wao mkuu ,Barbara Gonzalez na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Simba Sc,Mulamu Nghambi kukutana na kufanya mazungumzo na rais wa shirikisho la soka barani Afrika (CAF) Ahmad Ahmad makao makuu ya shirikisho hilo yaliyopo jijini Cairo,Misri.

Viongozi hao walianza ziara yao kwa kutembelea makao makuu ya klabu ya Al Ahly yaliyopo Cairo na kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo ya ufundi na uendelezaji wa wachezaji ikiwa ni kujenga kituo cha kukuza vipaji  kwa ushirikiano na timu ya Al Ahly.

Hawakuishia hapo bali waliendelea na ziara hiyo ya kikazi jijini Cairo kwa kutembelea pia makao makuu ya klabu ya Zamalek na kujadili mambo mengi na viongozi wa klabu hiyo ambayo yatawasaidia kupiga hatua katika soka.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited