Mashabiki wa klabu ya Simba sc sasa hawana budi kufurahi kufuatia kupona kwa beki wao mahiri Henock Inonga Baka ambaye alikua majeruhi baada ya kuumia katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union na kulazimika kuwa nje kwa takribani majuma mawili.
Beki huyo ameonekana yuko fiti katika kambi ya timu ya Taifa lake la Congo Drc ambapo ameonekana akishiriki mazoezi kujiandaa na michezo miwili ya kirafiki dhidi ya New Zealand siku ya Oktoba 13 na ule dhidi ya Angola Oktoba 18.
Beki huyo aliumiza mapema katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union baada ya kuchezewa rafu na mshambuliaji Hija Ugando ambapo alilazimika kukimbizwa hospitali na kushonwa jeraha hilo katika ugoko wake baada ya kuchanika na kulazimika kukaa nje kwa wiki mbili.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Simba sc ililazimika kuwatumia Che Fondoh Malone na Kennedy Juma katika michezo miwili dhidi ya Tanzania Prisons na Singida Fountain Gate ambayo yote miwili walipata ushindi uliwafanya wajikite kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini.