Mshambuliaji aliyekuwa anakipiga ndani ya Polisi Tanzania,Sixtus Sabilo ametambulishwa rasmi leo ndani ya Namungo Fc kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Sabilo amemaliza mkataba wake wa mwaka mmoja ndani ya Polisi Tanzania inayonolewa na Malale Hamsini hivyo ameamua kujiunga Namungo Fc akiwa kama mchezaji huru baada ya kuona mabosi wa Yanga Sc wapo kimya kwenye ahadi yao waliyomuahidi kuwa watamfuata baada ya ligi kumalizika ya msimu wa 2019/2020.