94
Baada ya Yanga kumpa siku 14, Papy Tshishimbi za kuamua hatma yake, jembe jipya kutoka Kagera Sugar, Zawadi Peter Mauya amesaini mkataba wa miaka miwili ili kuitumikia timu hiyo msimu ujao.
Mauya amesaini mkataba huo mbele ya mkurugenzi wa uwekezaji wa kampuni ya GSM inayoidhamini Yanga, Injinia Hersi Said, huku Kaimu Katibu wa Yanga, Wakili Simon Patrick akishuhudia.
Usajili wa kiungo huyo ni maandalizi kwa Yanga kujiandaa kuanza maisha mapya bila ya Tshishimbi ambaye kwa muda mrefu wamekuwa wakivutana katika suala la kusaini mkataba mpya.
Huu unakuwa usajili wa kwanza kwa Yanga kuelekea msimu ujao ambapo viongozi pamoja na wadhamini Kampuni ya GSM, wametamba kukisuka upya kikosi chao.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.