Home Makala Jezi za Simba SC septemba 4

Jezi za Simba SC septemba 4

by Sports Leo
0 comments

Mabingwa wa soka Tanzania Bara klabu ya soka ya Simba imetangazwa kuwa jezi mpya za timu hiyo kwaajili ya msimu wa wa 2021/2022 zitakazotumika kwenye michuano mbalimbali ya ndani na kimataifa zitazinduliwa rasmi tarehe 4 Sepetemba siku ya Jumamosi katika hafla itakayofanyika kuanzia saa 1-3 usiku jijini Dar es salaam.

Mtendaji mkuu wa Vunjabei Fred Ngajiro ambaye ndiye aliyeshinda zabuni ya utengenezaji na usambazaji wa jezi za timu hiyo amesema jezi hiyo itakuwa nzuri sana na ya kipekee.

Fred aliendelea kusema kuwa ”uzinduzi wetu wa jezi utakuwa Septemba 4 ,saa 1 usiku na jezi yetu itakuwa nzuri sana kushinda jezi za timu nyingine hizi za ndani”.

banner

”Baada ya uzinduzi jezi zitapatikana maduka yote ya Vunjabei nz zitauzwa masaa 24 na ninaamini kwamba ni bora,tumejitahidi kuzificha na zitaonekana kwa mara ya kwanza siku ya uzinduzi”.

Hizi ni harakati za Simba SC katika kuelekea tamasha kubwa la Simba day amabpo kilele chake kinatarajiwa kufanyika Septemba 19 katika dimba la Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba SC ina kazi ya kuwapiku watani wao wa jadi Yanga SC ambao jezi zao zimepokelewa vizuri na mashabiki na wadau wa soka nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited