Straika wa Simba Sc ,Meddie Kagere yuko hatarini kuikosa mechi ya watani wa jadi dhidi ya Yanga Sc kutokana na majeraha yanayomsumbua yatakayomfanya kukaa nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu ili apone kabisa.
Ikumbukwe kuwa mechi ya watani ilitakiwa kuchezwa leo,Octoba 18 lakini bodi ya ligi kuu Tanzania(TPLB) ikasogeza mbele na hivyo itafanyiika Novemba 7,2020 uwanja wa Mkapa.
Uongozi wa Simba Sc kupitia kwa Ofisa Habari,Haji Manara amesema kuwa,Kagere ameongezeka kwenye listi ya ya majeruhi kikosini kwao ambapo atakuwa nje kwa wiki tatu chini ya uangalizi maalum mpaka pale hali yake itakapotengemaa na kurejea uwanjani.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.