Klabu ya Kaizer Chiefs Fc imeonyesha kuvutiwa na mchezaji Maxi Nzengeli ambapo mabosi wa klabu hiyo wameanza mazungumzo na mabosi wa Yanga sc kumhitaji nyota huyo mzaliwa wa Kindu nchini Dr Congo ambaye Yanga sc ilimsajili msimu uliopita.
Nyota huyo licha ya kwamba ana mkataba wa mwaka mmoja na Yanga sc tayari mabosi wa klabu hiyo wameanza mchakato wa kumuongezea mkataba na wameshafungua mazungumzo na wakala wa mchezaji huyo juu ya dili hilo jipya.
Mpaka sasa msimamo wa mabosi wa Yanga sc ni kutomuacha staa huyo asajiliwe na timu nyingine ambapo wana malengo makubwa msimu huu ya kutwaa taji la ubingwa wa Afrika baada ya kunogewa msimu uliopita ambapo ilibaki kidogo wafuzu hatua hiyo kama sio makosa ya mwamuzi wa video kukataa bao la Aziz Ki.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Msimu huu pamoja na Yanga sc kuwaongeza mastaa wakubwa eneo la kiungo cha ushambuliaji lakini bado nafasi ya Nzengeli inaonekana kutokana na umuhimu wake kikosini hasa uwezo wake wa kushambulia na kukaba.