Kipa namba moja wa timu ya Taifa ya Tanzania na klabu ya Singida Fountain Gate Fc Beno David Kakolanya ana hatuhati ya kuukosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga sc siku ya ijumaa kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya kisigino kiasi cha kushindwa kushiriki mazoezi ya timu hio.
Mbali na Kakolanya pia mabeki Joash Onyango na Hamad Waziri pamoja na mshambuliaji Thomas Ulimwengu nao wana hatihati ya kuukosa mchezo huo kutokana na majeraha mbalimbali yanayowakabili kikosini humo hivyo mpaka sasa wana asilimia 50 pekee za kucheza.
Singida FG Itavaana na Yanga sc ijumaa jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa mchezo ambao timu zote zinahitaji alama tatu muhimu kujitengenezea mazingira ya ubingwa wa ligi kuu msimu huu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mpaka sasa Singida FG ipo katika nafasi ya tisa ya msimamo wa ligi kuu ikiwa na alama nane katika michezo sita huku Yanga sc ikiwa kileleni mwa msimamo ikiwa na alama kumi na tano katika michezo sita ya ligi kuu nchini.