Home Makala Kaze Kurithi Mikoba Ya Zlatico

Kaze Kurithi Mikoba Ya Zlatico

by Sports Leo
0 comments

Taarifa zinaeleza kuwa kocha mkuu,Cedric Kaze ndiye ambaye atarithi mikoba ya Zlatico Krmpotic ambaye alifutwa kazi rasmi Oktoba 3.

Zlatico alikiongoza kikosi cha Yanga kwenye mechi 8 ambapo katika hizo tano zilikuwa za ligi na tatu za kirafiki.

Kwenye mechi za kirafiki alishinda zote tatu na kwenye mechi za ligi kuu bara alishinda michezo minne huku akilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons.

banner

Mwenyekiti wa kamati ya usajili Yanga ambaye pia ni mkurugenzi wa uwekezaji ndani ya kampuni ya GSM ,Mhandisi Hersi Said ameweka wazi kuwa kocha mpya anaweza kutambulishwa hivi karibuni mambo yakisha wekwa sawa kwani anaweza akawa Kaze kwani ndio chaguo lao la kwanza japo alipata matatizo na akaomba udhuru.

Kwa sasa timu ya Yanga ambayo inajiandaa na mchezo wa dabi dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 18 ipo chini ya kocha msaidizi Juma Mwambusi wakimsubiri kocha wao mpya.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited