Rasmi sasa Mchezo wa KenGold dhidi ya Simba Sc utachezwa katika dimba la KMC June 18 japo hapo awali ilipangwa mchezo huo uchezwa katika dimba la Majimaji Mkoani Ruvuma.
Bodi ya ligi kuu wamejiridhisha kuwa uwanja huo bado haukidhi vigezo vya kutumika kwa michezo ya ligi kuu ya Nbc hivyo klabu ya KenGold itafute Uwanja mwingine kwakuwa dimba la Sokoine litakuwa kwenye matumizi ya mchezo wa Tanzania Prison dhidi Yanga sc katika siku hiyo hiyo.
Pamoja na juhudi mbalimbali zilizofanyika kuukarabati uwanja huo lakini uongozi wa Chama cha soka mkoa wa Ruvuma umegoma kuendelea kufanya marekebisho makubwa kisa mchezo mmoja wa ligi tu.
Kutokana na sababu hivyo basi imeamriwa kuwa mchezo huo sasa utachezwa katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam katika siku hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kurudishwa kwa mchezo huo kunatoa nafuu kwa Simba sc kutokana na kupunguza safari hivyo kuwafanya mastaa wa klabu hiyo kuwa na muda mzuri wa kujiandaa kwa ajili ya mchezo huo.