Home Makala Kipa Mpya Atua Simba sc

Kipa Mpya Atua Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kukamilisha usajili wa golikipa Ayoub Lakred aliyewahi kuzichezea klabu za Far Rabat na Rs Berkane ambazo zote zinashiriki ligi kuu ya Batola Pro ya nchini Morocco.

Kipa huyo mwenye miaka 28 amejiunga na Simba sc kwa mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru baada ya kukaa bila timu kwa takribani msimu mmoja tangu aachane na Far Rabat ambayo kwa sasa inanolewa na kocha wa zamani wa Yanga sc Nasredine Nabi.

Simba sc imeamua kumsajili Ayoub ili kuongeza ushindani katika eneo la golini hasa baada ya kuachana na kipa kutoka Brazil Jefferson Luiz kutokana na kuwa majeruhi aliyoyapata wakati wa kambi ya mafunzo ya msimu mpya (Pre-seasons) nchini Uturuki.

banner

Sasa Simba sc itakua na makipa wanne wa kikosi cha kwanza wakiwemo Aishi Manula,Ally Salim na Hussein Abel ambaye naye amesajiliwa msimu huu kutokea klabu ya Kmc.

Lakred katika klabu hiyo atakua ndie kipa mwenye wasifu mkubwa zaidi baada ya kufanikiwa kucheza michezo mikubwa na kunyakua makombe makubwa kama ya kombe la shirikisho barani Afrika pamoja na lile la ligi kuu ya soka nchini Morocco.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited