Home Makala Kipa Simba sc Matatani

Kipa Simba sc Matatani

by Sports Leo
0 comments

Kipa mpya wa klabu ya Simba sc Ayoub Lakred ni kama yuko matatani kufuatia mabosi wa klabu hiyo kuanza kufanya tathmini ya kiwango chake hasa baada ya kurejea kwa kipa Aishi Manula kikosini humo.

Mabosi wa klabu hiyo walikua na matumaini makubwa na kipa huyo wa zamani wa Far Rabat mabingwa wa ligi kuu nchini Morocco lakini kufungwa mabao ya kizembe hasa katika michezo ya kimataifa dhidi ya Power Dynamos kumeanza kuwafikirisha kumtema katika usajili wa dirisha dogo mwezi januari.

Kipa huyo katika michezo miwili ya kimataifa dhidi ya Power Dynamos alifungwa jumla ya mabao matatu huku mawili akifungwa ugenini na moja nyumbani hali iliyoanza kuwa wasiwasi mabosi hao huku wakiona kabisa kuwa atawekwa benchi na Aishi Manula pindi atakapokua fiti jambo ambalo sio zuri kwa kipa wa kimataifa kuwekwa benchi na mzawa.

banner

Simba sc italazimika kauchana na kipa huyo iliyemsajili msimu huu ili kuwapa nafasi vijana Ally Salim na Hussein Abel kumsaidia Aishi Manula katika michuano mbalimbali klabuni hapo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited