Mshambuliaji wa Manchester City nchini Uingereza, Sergio Aguero amesema kuwa wanahofia kurejea uwanjani wakati huu ambapo janga la Covid-19 halijadhibitiwa vilivyo takribani mataifa yote duniani .
Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) ilitarajiwa kuendelezwa mnamo Juni 8 hali ambayo ingehitaji wachezaji kurudi mazoezini kikamilifu kufikia Mei 18.
Vinara wa vikosi vyote 20 vya EPL wanatazamiwa kukutana leo Ijumaa ya Mei 1, 2020 kujadili njia mbalimbali za kurejelewa kwa kampeni za muhula huu .
“Wachezaji wengi wanaogopa kurejea uwanjani kwa sababu wana watoto na familia ambazo zinawategemea pakubwa” alisema Aguero, wakati akihojiwa na runinga ya El Chiringuito nchini Argentina.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Nyota huyo mwenye kuzifumania nyavu aliongeza kuwa wachezaji wengi wanasema kuna watu walio na virusi vya corona ila hawaonyeshi dalili zozote za ugonjwa huo hivyo itakuwa rahisi sana kwa watu kuambukizana iwapo watarejea uwanjani ikiwa hali si shwari.