Klabu ya Young Africans Sc imetozwa faini ya laki tano (500,000) kwa kosa la mashabiki wa timu yake kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu kwa kuwapiga na kuwachania jezi mashabiki wanaohisiwa ni wa timu ya Simba Sc waliokuwa wamevaa jezi za simba kwenye mchezo uliochezwa Septemba,27 kati ya Mtibwa Sugar na Yanga Sc kwenye uwanja wa Jamuhuri jijini Morogoro.Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 45:1 ya ligi kuu kuhusu udhibiti wa klabu.
Mashabiki wawili wa yanga sc wanaofahamika kwa majina maarufu kama Osama na Jesca wamefungiwa kuingia uwanjani kwa kipindi cha miezi 12 kwa kosa la tukio la kushiriki kuwapiga na kuwachania jezi mashabiki waliokuwa wamevaa jezi za Simba Sc wakihisiwa kuwa ni wa timu hiyo iliyochezwa Septemba 27,2020 uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro.
Katika kufanikisha maamuzi hayo picha za mashabiki hao zitabandikwa magazeti yote ya viwanja vinavyotumika kwa michezo ya ligi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Adhabu hii imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 45:2 ya ligi kuu bara kuhusu udhibiti wa klabu.