Home Makala Kisinda Ruksa Yanga sc

Kisinda Ruksa Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imeruhusiwa na kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kumtumia winga Tuisila Kisinda ambaye imemsajili kwa mkopo akitokea klabu ya Rs Berkane ya nchini Morroco baada ya hapo awali kuzuiliwa na Shirikisho la soka nchini (TFF) kwa minajiri ya kwamba usajili huo umefanyika bila kuzingatia kanuni za usajili wa wachezaji wa kigeni nchini.

Yanga sc ilikwama kumtumia mchezaji huyo katika michezo dhidi ya Azam Fc na Mtibwa Sugar kutokana na kizuizi hicho lakini taarifa rasmi kutoka TFF imethibitisha kuruhusiwa kwa mchezaji huyo aliyeingizwa katika usajili akichuka nafasi ya Lazarus Kambole ambaye ni majeruhi na anahitaji muda mrefu ili kurudi katika ubora wake.

Taarifa hiyo pia imethibitisha kuwa Kambole tayari ametolewa kwa mkopo kwenda Wakaso Giants ya nchini Uganda na kuiacha Yanga sc ikiwa na wachezaji 12 wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za usajili wa wachezaji wa kigeni.

banner

Kisinda anarejea Yanga sc ambayo ilimuuza msimu mmoja uliopita kwenda Rs Berkane ambapo ameshinda taji la kombe la shirikisho barani Afrika na sasa anarejea jangwani baada ya kocha mpya wa klabu hiyo ya Rs Berkane kutomhitaji kikosini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited