Home Makala Klopp Alishawahi Kulewa Hadi Kupoteza Kumbukumbu

Klopp Alishawahi Kulewa Hadi Kupoteza Kumbukumbu

by Sports Leo
0 comments
Liverpool Manager Jurgen Klopp - Sports Leo sportsleo.com

Kocha Mkuu wa Liverpool,Jurgen Klopp amesema kuwa hakumbuki chochote juu ya klabu ya Borussia Dortmund ilipokutwaa ubingwa wa Bundesliga msimu wa 2011/12 kwani wakati wa sherehe alikuwa amelewa chakari mpaka kupoteza kumbukumbu.

Klopp kwa sasa ni miongoni mwa makocha wenye majina makubwa duniani na alitengeneza jina lake alipojiunga Dortmund mwaka 2008 hata ilipotwaa ubingwa walishangalia sana hadi kumfanya anywe sana pombe na kupoteza kabisa kumbukumbu za namna sherehe za ubingwa zilivyokuwa msimu wa 2012.

Kwa sasa Klopp anapambana ndani ya Liverpool inayoshiriki Ligi Kuu England huku ikipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa pale ligi itakaporejea kwani imesimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona na taarifa zinaeleza itaanza Juni Mosi bila uwepo wa mashabiki uwanjani.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited