Home Makala Kocha Mpya Yanga Sc Balaa

Kocha Mpya Yanga Sc Balaa

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imemtambulisha kocha Roman Folz raia wa Ufaransa kama kocha mkuu wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Miloud Hamdi aliyemaliza mkatab klabuni hapo.

Folz ametambulishwa klabuni hapo akiwa na kazi ngumu ya kuhakikisha makombe hayakauki klabuni hapo baada ya msimu huu kuchukua mataji matano yakiwemo ya ligi kuu na kombe la Shirikisho la Crdb nchini.

Folz mwenye miaka 35 alikua kocha msaidizi wa klabu ya Mamelodi Sundowns ya nchini Afrika ya kusini huku akiwahi kuwa kocha mkuu mara kadhaa kwa baadhi ya klabu ikiwemo Shekhukune United ya nchini Afrika ya kusini.

banner

Hata hivyo historia ya Folz inaonyeshwa kuwa huwa hadumu kama kocha mkuu kwa zaidi ya mwaka mmoja huku ukocha msaidizi akiwa amefundisha kwa muda mrefu zaidi.

Pia aliwahi kufanya kazi katika Shirikisho la Soka duniani (Fifa) huku pia akiwa na leseni ya Uefa Pro License inayompa sifa zote za kufundisha ligi kuu ya Nbc nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited