Home Makala Kramo Wiki Tatu Nje

Kramo Wiki Tatu Nje

by Sports Leo
0 comments

Kiungo Mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Ivory Coast Aubin Kramo anatarajia kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki 2 hadi 3 akiuguza Jeraha lake la goti alilolipata hivi karibuni katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ngome Fc.

Kramo ameomba ruhusa kwa uongozi wa klabu ya Simba aende kwao kujitibu jearaha hilo pamoja na kujiweka sawa kisaikolojia ambapo atarejea kuanzia  mwezi wa Kumi kwa ajili ya kuanza kuitumikia timu hiyo.

Kramo amekua na wakati mbaya klabuni hapo ikiwa mpaka sasa hajacheza mechi yeyote iliyo ya mashindano kutokana na majeraha hayo tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea klabu ya Asec Mimosas ya nchini kwa Ivory Coast.

banner

Kikosi cha Simba sc tayari kimewasili jijini Ndola nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wa kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika wakitarajiwa kukutana na Power Dynamos ya nchini humo ambapo mshindi wa jumla atafuzu hatua hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited