Waandaaji wa mbio za Bunge Marathon wamesema wameandaa mpango maalumu wa kukuza mchezo wa riadha kupitia mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika hivi karibuni April 12 2025 jijini Dodoma.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Mwenyekiti wa michezo wa Bunge Mh.Festo Sanga alisema kuwa fedha zitakazopatikana mwaka huu zitatumika kujenga shule ya wavulana ya Bunge katika eneo la Kikumbi jijini Dodoma.
“Bunge la Tanzania limeshajenga Shule ya Sekondari ya Wasichana katika eneo la Kikombo, jijini Dodoma na sasa hivi tunashirikiana na watanzania kupitia Mbio hizi kujuenga Shule ya Sekondari ya Wavulana jijini Dodoma. Hivyo nawaomba watanzania mjitopkeze kwa wingi kushiriki katika mbio hizi alisema Mh.Sanga ambaye ni mbunge wa Makete.
“Mchango wa mbio za marathon utasaidia sekta ya elimu utaongozwa na Waheshimiwa Wabunge huku ikiambatana na dhamira ya Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukuza michezo na elimu, mbio hizi pia zinatoa fursa kwa Wabunge kuimarisha uhusiano wao na Watanzania sambamba na kuendeleza utimamu wa mwili na kuishi kiafya.” Amesema Mh.Sanga
Akizungumzia kuhusu zawadi kwa washindi Mheshimiwa Sanga amesema kwenye nusu marathon yaani kilometa 21, mshindi wa kwanza atajinyakulia Milioni 5, mshindi wa pili atapata Milioni 3 na mshindi wa tatu akiambulia Milioni 1.5.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kwa upande wa kilomita 10, mshindi wa kwanza atazawadiwa shilingi milioni 2, mshindi wa pili Shilingi 1.5, na mshindi wa tatu atajinyakulia shilingi milioni moja huku. Katika kilomita 5 mshindi wa kwanza atapata shilingi 1.5, nafasi ya pili akipata milioni moja na mshindi wa tatu atapata shilingi laki tano.
Mbio hizo zitafanyika katika umbali wa kilomita kuanzia 5,10 na 21 huku kujiandikisha ikiwa ni shilingi za kitanzania elfu arobaini ambapo fedha hizo zitakazopatikana zitatumika kujenga shule ya Wavulana ya Bunge jijini Dodoma eneo la Kikombo.
Mbio za Bunge marathon zitafanyika Aprili 12 , 2025 zikiwa na matarajio ya kuvunja rekodi ya kuwa na washiriki zaidi ya 5,000kutoka ndani na nje ya nchi.