Juventus wameinamishwa kichwa chini baada ya kufungwa bao 1-0 na Lyon katika mchezo uliosimamiwa na refa Jesus Gil kutoka Spain katika uwanja wa Groupama Stadium.
Bao la ushindi wa kipekee kutoka Lyon lililodumu hadi dakika 90 za mchezo lilifungwa kupitia Lucas Tousart dakika ya 31.
Lyon hawakuachwa nyuma kupewa kadi ya njano kwa wachezaji wake wawili ambao ni Marcelo dakika ya 28 na dakika ya 61 Maxwel Cornet huku Juventus wakiwa wameponea chupuchupu.